Kuhusu Jumuiya Zawiyatul Qadiriya Tanzania
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu (S.W) kwa kutupa uzima na afya pamoja na kutujaalia uwezo wa kupata Jumuiya yetu hii, JUMUIYA ZAWIYATUL QADIRIYA TANZANIA. Ili kudumisha umoja wetu KI-DINI katika misingi imara zaidi, tumeamua kuunda Jumuiya ya kutuwezesha kuendeleza umoja wetu kihalali kwa faida zetu, vizazi vyetu vya sasa na vya baadaye na Waislamu wote.
Jumuiya ilianza jitihada zake tangu mwaka 1980 na ikasajiliwa rasmi mwaka 1992, chini ya uongozi na malezi ya mwasisi wetu, Sheikh Muhammad Nassor. Jumuiya inaendesha shughuli zake kupitia mikoa, matawi na vituo mbalimbali nchini Tanzania, ikijumuisha elimu ya dini, matukio ya kijamii, uratibu wa mali za jumuiya (misikiti na zawiya), pamoja na huduma za kifedha kwa maendeleo ya wanachama.
Tunachofanya
Elimu
Madrasa, Maahad, na mipango ya ufadhili wa masomo (Scholarships).
Uendeshaji
Ujenzi wa misikiti, madrasa, nyumba pamoja na miradi ya maendeleo.
Mengineyo
Huduma za Hijja, Zakka, Sadaka, misaada ya mayatima na uchimbaji wa visima.
Dira, Malengo na Dhamira
Dira
Kumjua Mola wetu na kupata radhi zake kupitia malezi ya Twariqa.
Malengo
Kumjua Mola wetu (S.W) na kupata radhi zake: ufanisi wa uendeshaji, uendelevu wa kifedha, elimu ya Shariah, afya na mazingira, na huduma bora kwa jamii.
Dhamira
Kuwa na mwenendo wa kutekeleza shughuli za ibada za kimwili na kiroho.