Tunamshukuru Mwenyezi Mungu (S.W) kwa kutupa uzima na afya pamoja na kutujaalia uwezo wa kupata Jumuiya yetu hii, JUMUIYA ZAWIYATUL QADIRIYA TANZANIA. Ili kudumisha umoja wetu KI-DINI katika misingi imara zaidi, tumeamua kuunda Jumuiya ya kutuwezesha kuendeleza umoja wetu kihalali kwa faida zetu, vizazi vyetu vya sasa na vya baadaye na Waislamu wote.
Katika zama hizi tulizonazo, hali halisi ya Waislamu katika elimu ya Dini, Imani, ucha Mungu, na uongozi wa Dini ni duni sana. Kwa hiyo, sisi wafuasi wa Twariqa ya Qadiriya hapa Tanzania tumeamua kujitambulisha rasmi kwa Serikali zetu na kwa Waislamu wenzetu kote nchini.
Ili kufanikisha nia hiyo, na kufuatana na sheria ya nchi yetu, tumejiandikisha kama Jumuiya rasmi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kutambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mategemeo yetu ni kwamba chombo hiki kitakuza na kuimarisha mapenzi na mashirikiano mema baina yetu na Waislamu wengine popote walipo.
Lengo letu Waislamu sote ni moja: kufuata kumjua Mola wetu na kupata radhi zake. Jumuiya yetu hii ni ya KI-DINI na imejengwa juu ya maadili ya Qur’ani na Sunna za Mtume Muhammad (SAW).
Juhudi za kuiandikisha Jumuiya zilianza mwaka 1980 na baadaye kufanikishwa rasmi mwaka 1992. Leo hii, JZQT inaendelea kuimarisha malezi ya kiroho, maadili, na mshikamano wa jamii.
Muanzilishi: Sheikh Muhammad Nassor
Huduma zenye mchango wa kijamii, kielimu na kiroho
Madrasa, Maahad, na mipango ya ufadhili wa masomo (Scholarships) kwa maendeleo ya elimu bora.
Ujenzi wa misikiti, madrasa, nyumba pamoja na miradi ya maendeleo kwa ustawi wa jamii.
Huduma za Hijja, Zakka, Sadaka, misaada ya mayatima na uchimbaji wa visima.
Msingi unaotuongoza katika kazi, ibada na maendeleo ya Jumuiya
Kumjua Mola wetu na kupata radhi zake kupitia malezi ya Twariqa.
Kumjua Mola wetu (SW) na kupata radhi zake.
Kuwa na mwenendo wa kutekeleza shughuli za ibada za kimwili na kiroho kwa njia bora, nyepesi na ya haraka, zinazojenga tabia njema na kuleta maendeleo endelevu ndani ya Jumuiya.
© www.jzqt.or.tz
Template Design: HTML
Codex