Zanzibar, Tanzania +012 345 6789 info@jzqt.org
Wanajumuiya

3453

Vituo

20

Zawiya

409

Habari/Taarifa

Taarifa ya matukio mbali mbali

JZQT?

Taarifa kuhusu Jumuiya

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu (S.W) kwa kutupa uzima na afya pamoja na kutujaalia uwezo wa kupata Jumuiya yetu hii, JUMUIYA ZAWIYATUL QADIRIYA TANZANIA. Ili kudumisha umoja wetu KI-DINI katika misingi imara zaidi, tumeamua kuunda Jumuiya ya kutuwezesha kuendeleza umoja wetu kihalali kwa faida zetu, vizazi vyetu vya sasa na vya baadaye na Waislamu wote.
Katika zama hizi tulizonazo, hali halisi ya Waislamu katika elimu ya Dini, Imani, ucha Mungu, na uongozi wa Dini ni duni sana. Kwa hiyo, sisi wafuasi wa Twariqa ya Qadiriya hapa Tanzania tumeamua kujitambulisha rasmi kwa Serikali zetu na kwa Waislamu wenzetu kote nchini. Ili kufanikisha nia hiyo, na kufuatana na sheria ya nchi yetu, tumejiandikisha kama Jumuiya rasmi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kutambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mategemeo yetu ni kwamba, chombo hiki kitakuza na kuimarisha mapenzi na mashirikiano mema baina yetu na Waislamu wengine popote walipo.
Lengo letu Waislamu sote ni moja: kufuata kumjua Mola wetu na kupata radhi zake. Jumuiya yetu hii ni ya KI-DINI. Hivyo tumetengeneza Katiba hii katika misingi ya maadili ya Qur’ani na Sunna za Bwana Mtume Muhammad (SAW). Juhudi za kuiandikisha Jumuiya yetu hii zilianza katika mwaka 1980. Kwa bahati mbaya hatukufanikiwa wakati huo. Lakini Mwenyezi Mungu (SW) amejaalia, kwa bidii na juhudi za ndugu zetu wa Arusha, tumeweza kuandikishwa.
Tulianza kwa kuandikisha udhamini kwa jina la MASJID ZAWIYA EL-QADIRIYA AND ISLAMIC CENTRE mnamo tarehe 7/1/1988 na kutangazwa katika gazeti rasmi la Serikali. Jitihada ziliendelea kufanywa na ilipofika mwaka 1990, tukafanikiwa kukiandikisha chombo hiki Wizara ya Mambo ya Ndani na kupewa Hati ya kuandikishwa Nambari S.O.7168 ya tarehe 2/11/90. Katika Mkutano Mkuu wa kwanza uliofanyika tarehe 26/9/91 hadi 29/9/91 huko Arusha, wajumbe katika kujadili Katiba, walikubaliana kubadili jina ili chombo hiki kitambulikane kuwa ni cha nchi nzima. Jina jipya lililokubaliwa lilikuwa JUMUIYA ZAWIYATUL QADIRIYA TANZANIA (yaani Jumuiya ya Mazawiya ya Twariqa ya Qadiriya hapa Tanzania).
Tarehe 10/4/1992, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa Hati nyingine ya uandikishaji nambari S.O.7168 kwa jina jipya. Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu wa Wadhamini nayo tarehe 9/11/1992 ilitoa Hati mpya kwa jina jipya na kutangaza katika gazeti la Serikali la tarehe 27/11/1992 ukurasa 937, tangazo nambari 947.
Misingi na chanzo cha Jumuiya hii inatokana na Twariqa. Kwa miaka mingi sasa tangu Uislamu uingie katika nchi yetu (Al-Hamdulillah) mafunzo ya Twariqa yamekuwa yakitolewa na Mashekhe mbalimbali na taratibu zake za Ibada zimekuwa zikifuatwa. Lakini kutokana na hali ya ulimwengu ulivyo na nyoyo kumili katika ulimwengu tukaonelea iko haja kuzidi kukumbushana katika Dini yetu. Hivyo, katika mazingira ya aina hii, imebidi tuzidishe bidii katika kuzisafisha nafsi zetu kwa kushikamana na Twariqa. Muanzilishi na muasisi wa JZQT ni shekhe Muhammad nassor

Huduma Zetu

Tunazoshughulikia

Elimu

Madrasa, Maahad, Scholarship(Ufadhili wa Masomo)

Uendeshaji

Ujenzi wa Misikiti, Madrasa, Nyumba

Mengineyo

Hijja, Zakka, Sadaka, Mayatima, Visima

Mwelekeo

Dira, Malengo na Dhamira

Dira

Yetu

Kumjua Mola wetu na kupata radhi zake kupia malezi ya Twarika.

Malengo

Yetu
Lengo Kuu

Kumjua Mola wetu (SW) na kupata radhi zake.

Malengo mahususi
  • Kukuza Ufanisi katika Uendeshaji wa Shughuli za Jumuiya
  • Kuimarisha Upatikanaji wa Fedha na Mipango
  • Kukuza Elimu ya Shariah na Malezi ya Twariqa
  • Kuimarisha Afya na Mazingira bora kwa Wanajumuiya na jamii
  • Kutoa Huduma nyenginezo zilizo bora na endelevu

Dhamira

Yetu

Kuwa na mwenendo wa kutekeleza shughuli za ibada za kimwili na kiroho kwa njia iliyo bora, nyepesi nay a haraka zenye kujenga tabia njema na kuleta maendeleo katika Jumuiya.




Wasiliana Nasi

Zanzibar, Tanzania

info.jzqt.org

+012 345 67890

© www.jzqt.org - Haki zote Zimemilikiwa. Template by HTML Codex